SHENG CORNER

Valentine's Day ya ma red rose

Fans urged to express love to family and kids, not just their partners

In Summary

• From a lavish dinner to comedy to romantic plans, celebs share their plans

Rose flowers on display at the City market in Nairobi as the world marked Valentines day.
VALENTINES Rose flowers on display at the City market in Nairobi as the world marked Valentines day.
Image: File

Wasee, leo ndio ile siku ya kushare malavi davi, kwa kifupi Valentine. Well, ingawa ni siku ya janta, najua mraiya mmeplan evening mtakua maeneo kadhaa mkicelebrate na mtu wa yours.

Majamaa najua mmeplan kupeleka ma red rose ama maroro wenu for a date, ama pia kuspend kwa tujoints twa ndogogio. Kwa hii indaa ya macelebs, tumebonga na kadhaa.

Size 8 na msee wa kwake DJ Mo watakua na couple's dinner pale Emory. Si mmecheki vile wamekua wakibonga ju ya hiyo riba? Size 8 amesema dinner ni miti saba kwa ma morio ordinary na miti kumi kwa ma VIP.

 
 
 

Msanii Ben Githae, yule wa 'Tano Tena', amaedai kuwa atakua pale Blue Spring na ma arif wengine wa industry. Pia amesema Vale ni siku ke express love kwa kila msee, sio lazima akue wa ngoro. Amedai kuwa unaeza fanyia Mathe pale mushatha kitu, ma junia wako ama pia utembelee watoi yatima.

Rose flowers
Rose flowers
Image: File

"Valee ni dei ya kujijua na kuchapiana maristo ndio tujue mavita zinafanyika chini ya waba," alisema. Amedai pia ataungana na mandume wenzake kwa ile shughuli yao (men's confrence) kama itafanyika.

Pastor Nganga amedai atakua akiombea nchi, na akimada atakua na mama wa kwake wakitafta watoto... "Vale nitakua Kajiado kwa maombi. Tuko na Watoi but tutaongeza kegine hiyo day," Nganga alidai.

Njugush na mama wa kwake Wakavinye watakua pale Garden City kufanya shughuli zao za Ucheshi.

Ni muhimu kama mavijanaa tukae rada tusijiingize kwa ngori ya masanse ama marhino hiyo day. Kula raha yako ndogo ndogo na usisahau kuna future, msee. Kama huna mamaa na machetha/maweng', pia haina noma, na usiteteveve.

Cheza na ligi yako.